Habari za Punde

JKU yairusha roho KVZ

Na Mwajuma Juma

MABANATI wa maafande wa JKU na Sogea, wameanza vyema ligi ya netiboli kanda ya Unguja baada ya kushinda katika michezo yao iliyochezwa juzi kwa nyakati tafauti.

Wajenga uchumi wa JKU ambao walishuka katika dimba la Gymkhana wakati wa saa 9:30, waliwatoa nishai ndugu zao wa KVZ kwa kuwachapa mabao 47-36, huku Sogea wakiishushia Tuko imara kipigo cha mabao 36-25 katika mchezo uliofuatia.


Hata hivyo, KVZ iliweza kuongoza katika robo ya kwanza kwa mabao 10-9, kabla dada zao wa JKU kuzinduka ikiwatumia wafungaji wake Masika Kombo na Zainab Shaibu, kuwamaliza Valantia hao, hasa baada ya kumuingiza Pili Peter kuchukua nafasi ya Masika Kombo.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo uwanjani hapo kwa michezo
miwili, ambapo wakati wa saa 9:30, Zimamoto itaikabili Ikulu, na saa 10:45 Mafunzo watakuwa vitani dhidi ya maafande wa Nyuki yote ni kwa upande wa wanawake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.