Habari za Punde

Mheshimiwa Raza Amwaga Vifaa vya Mamilioni Jimboni Kwake Uzini Zenj

 Vifaa vya kusambazia maji katika Jimbo la Uzini vilivyotolewa na Mhe Raza kwa maeneo ya jimbo hilo, ambayo yana uhaba wa upatikasnaji wa Maji Safi na Salama katika Vijini vya Umbuji, Kiboje Mazese, Miwani na Kiboje, vikiwa katika uwanja wa mpira Mazese. vikisubiri kukabidhiwa wahusika kwa ajili ya kufanyia kazi ya usambazaji maji katika maeneo ya jimbo hilo, kama alivyotowa ahadi yake kutatua suala hilo maji.
 Mipira kwa ajili ya timu za Jimbo la Uzini kwa timu 25 za Jimbo hilo.
 Mahela ya Vikundi vya Wanawake wa Jimbo hilo zilizotolewa na Mhe Raza, ikiwa ni ahadi yake wakati wa Kampeni kuinua hali ya Uchumi kwa Vikundi vya Ushirika vya Jimbo la Uzini, jumla ya Vikundi 57 vimefaidika na pesa hiz, kila kikundi kimepata shilingi laki mbili.
Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Ali Hassn Mwinyi, akisalimiana na Viongozi wa Chama na Serikali alipowasili katika sherehe za kukabidhi Vifaa kwa Wananchi wa Jimbo la Uzini vilivyotolewa na Mhe Mahammed Raza, zilizofanyika katika uwanja wa mpira wa mazese kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mhe Mohammed Raza akimtambulisha mtoto wake  Hassan kwa Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi, katika viwanja vya mpira mazese kiboje wakati wa sherehe za kukabidhi vifaa vya Jimbo la Uzini Unguja.

 Mhe Rais Mstaaf wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Haji Ussi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na kushoto Mwakilishi wa Uzini Mohammed Raza Hassanali na Mbuge Mohammed Seif Khatib, wakiwa katika viwanya vua sherehe hiyo wakiwasikiliza wasoma utenzi.   

 Dodo na Amani wakisoma utenzi katika sherehe za kukabidhi Vifaa vya Jimbo la Uzini vilivotolewa na Mhe Raza ikiwa ni kutimiza ahadi yake na Ilani ya Chama cha Mapinduzi, kuwapatia Wananchi huduma bora.  
 Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi, akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Jimbo Uzini, katika sherehe za kukabidhi Vifaa vya Jimbo hilo vilivyotolewa na Mhe Raza.    
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magaribi Abdalla Mwinyi Khamis, akitowa salamu za Mkoa huo kwa Mhe Rais Mstaaf wa Tanzania Ali Hassn Mwinyi, kwa wananchi wa jimbo hilo.   
 Wananchi wa jimbo la Uzini wakimshangiria Mwakilishi wao akiwahutubia katika sherehe za kuwakabidhi vifaa kwa ajili ya jimbo lao.
 Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo lake kutimiza ahadi alioitowa wakati wa kampeni za Uchaguzi mdogo uliofanyika jimboni humo.

Wananchi wakishangiri wakati Mzee Ruhusa Mhe Ali Hssan Mwinyi akiwahutubia katika Mkutano wa kukabidhi Vifaa vya Jimbo hilo.  

Mhe Mohammed Raza, akimkabidhi CD Rais Mstaaf wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, ya mikutano yake yote ya kampeni na ahadi alizozitowa kwa Wananchi wa Jimbo lake la Uzini na tayari ameshaaza kutimiza ahadi hizo kwa vitendo.


 Mbuge wa Uzini Mohammed Seif Khatib akiwahutubia wnanchi wa Uzini. 
 Bi Naila Jidawi akiwa katika Mkutano wa kukabidhi Vifaa kulia Hassan Mohammed Raza na kushoto Mama Hassan wakiwa katika mkutano huo. 
Mhe Rais Mstaaf wa Tanzania akionesha Kifaa cha moja ya Hospitali za Jimbo hilo baada ya kukabidhiwa na Mhe Mohammed Raza, ili kukabidhi kwa Wafanyakazi wa Vituo vya Afya vilioko katika jimbo hilo kulia Mbuge Mohammed Seif Khatib.jumla ya Vituo vitano vitafaidia na vifaa hivyo Umbuji, Kiboje, Uzini Miwani na Mchangani vilioko kaqtika Jimbo hilo.

Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Ali Hassn Mwinyi, akimkabidhi mmoja wa Wafanyakazi wa Vituo vya Afya vya Jimbo hilo, kifaa cha kupimia Presha.

Mhe Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi mipira mwakilishi wa timu hizo akipoke kwa niaga ya timun zote mipira iliotolewa na Mwkilishi wa Jimbo hilo Mhe Mohammed Raza.
Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi Fedha mwakilishi Zena Seif wa Vikundi 57  vya Ushirika katika jimbo hilo shilingi laki mbili kila kikundi.  
 Rais Mstaaf wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Vifaa kwa ajili ya kusambaza Maji safi na Salama Mkurugenzi Ufundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Mohammed Elias, ili mkuaza kazi hiyo ya usabazaji wa maji katika jimbo hilo, kushoto Mwakilishi wa jimbo hilo Mohammed Raza.    
 Rais Mstaaf wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Vifaa kwa ajili ya kusambaza Maji safi na Salama Mkurugenzi Ufundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Mohammed Elias, ili mkuaza kazi hiyo ya usabazaji wa maji katika jimbo hilo 
 Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza, akizungumza na Waandishi wa habari baada ya sherehe za kukabidhi Vifaa kwa ajili ya Jimbo lake alivyotoa ahadi kwa Wananchi wake. 
Wananchi wa Jimbo la Uzini wakimshangira Mwakilishi wao kwa kutimiza ahdi aliowapa za kutatu matatizo yote yanayolikabili jimbo lao baada ya kushinda Uchaguzi Mdogo w jimbo uliofanyika miezi iliopita na kuibuka mshindi. 

1 comment:

  1. Si mchezo nawapongeza wananchi wa uzini kwa kutosikiliza fitna za walafi wachache na wakamchaguwa mtu sahihi ambae ni dira ya maendeleo ya jimbo lao, majimbo mengine yafuate mifano wa uzini nawasihi wazanzibari tuache kuangalia chama cha mgombea bali tuangalie utendaji wa mtu mwenyewe. Mfano sahihi ni huyo Mohammed Seif Khatib yupo mwaka wa 30 hapo jimboni kama sikosei ila hajafanya jambo lolote la maana, nadhani pia kwenye ubunge tunahitaji kufanya maamuzi sahihi pia

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.