Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 13/7/2012 .
Serikali ya Zanzibar inatarajia kuanzisha mfuko wa bima ya afya ili kuweza kuwaondolea usumbufu
wa tiba wananchi wake .
Hayo yamesemwa katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi na Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Sira Ubwa Mamboya wakati akijibu suala la Jaku Hashim Ayoub
Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni aliyetaka kujua uanzishwaji mfuko wa bima ya afya
kwa Zanzibar.
Dk. Sira alisema kwamba uanzishwaji wa
huduma ya bima ya afya kwa Zanzibar
ni tayari na hivi sasa iko katika hatua za awali za kufanya tafiti za kuweza
kujua utayari wa uwezo wa wananchi .
Alisema kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
imeshawapatia mafunzo wafanyakazi wa Wizara ya afya Zanzibar juu ya jinsi ya
kuendeleza mfuko huo kwa hospitali zote za serikali Binafsi na NGO kwa unguja na Pemba .
Dk. Sira alisema mfuko wa bima ya afya ya Zanzibar umeshafungua
ofisi yake na kuweza kuwajiri wafanyakazi wake wakiwemo daktari, muhasibu, na dereva
.
Aidha alisema kuwa tumaini ni kwamba mfuko
huo utafanyakazi vizuri kwa lengo la kuziwezesha hospitali za Serikali za
Unguja na Pemba ziweze kunufaika na huduma
hiyo.
Akieleza dhamana ya uazishwaji wa mfuko huo
alisema itasimamiwa na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kwa upande wa mfuko wa bima wa
taifa,alisema tayari umeanza kufanya kazi zake Zanzibar kuanzia mwaka 2007 na una jumla ya
wanachama 5,393 ukichanganya pamoja na familia zao idadi inafikia 28,044 wanafaidika na mfuko huo.
No comments:
Post a Comment