Habari za Punde

Uzinduzi wa kituo cha mkono kwa mkono Chakechake Pemba


Waziri wa Ustawi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohamed alikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Mkono kwa Mkono (One sto Centre) huko Hospitali ya Chake chake Kisiwani Pemba jana

Viongozi mbali mbali wa taasisi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa kituo cha Mkono kwa Mkono (One sto Centre) huko Hospitali ya Chake chake Kisiwani Pemba jana wakimsikiliza Waziri wa Ustawi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zazinab Omar Mohamed akitoa hutuba yake kwa wananchi

Mwakilishi kutoka Shirika la Save the Children Mubaraka Maman, akitoa maelezo machache kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha Mkono kwa mkono huko hospitali ya Chake chake Kisiwani Pemba ambapo shirika hilo limechangia kwa asilimia kubwa kufanikisha ktuo hicho

 Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Fatuma Gharib akitoa maelezo juu ya kuanzishwa kwa kituo hicho na kile kilichopo Unguja kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha Mkono kwa mkono huko hospitali ya Chake chake Kisiwani Pemba jana
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Major Mstaafu Juma Kassim Tindwa akizungumza na wananchi kabla ya kumkaribisha Waziri Zainab katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha Mkono kwa mkono huko hospitali ya Chake chake Kisiwani Pemba jana

Waziri wa Ustawi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zainab Zanzibar Omar Mohamed akizungumza na wananchi wa Pemba mara baada ya uzinduzi wa kituo cha mkono kwa mkono huko Hospitali ya Chake chake Kisiwani Pemba, kushoto mwenye miwani Afisa Mdhamini Wizara hiyo Pemba Mauwa Makame Rajabu akifutiwa na Afisa Tawala Mkoa wa Kusini pemba Hanuna Ibrahim Massoud

Picha zote na Haji Nassor, Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.