Na Salama Salim Pemba .
Katika kuwafariji wahanga wa waliofikwa na janga la
moto katika maeneo tofauti ya kijiji cha Tumbe wilaya ya Micheweni Mkoa wa
kaskazini Pemba ,wametakiwa kuwa na moyo wa
subira katika kipindi hiki kigumu kilichowakumba miongoni mwao.
Hayo yameelezwa jana na Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri wa
Wilaya ya Micheweni, Kombo Hassan Khamis kwa niaba ya Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo Abdalla Ali Said wakati alipokuwa akizungumza na wahanga wa ajali hiyo
huko kijijini kwao.
Alisema kuwa kutokana na janga la moto huo ulioingia katika
kijiji cha Tumbe mashariki umekuwa ni wakushangaza sana hali ambayo imeleta mfadhaiko mkubwa
wakaazi wanaoishi maeneo hayo.
Alifahamisha kuwa kutokana na janga hilo
halmashauri ya wilaya ya micheweni itachukuwa hatuwa za maksudi kwa ajili ya
kuwasaidia wale wote ambao wamepatwa na janga hilo .
“kutokana na janga hili la kushangaza kwa wahanga hawa
halmashauri hii haina budi kuchukuwa hatuwa za makusudi kwa ajili ya kuwasaidia
wale wote ambao wameathirika”,alifahamisha Mwenyekiti huyo.
Nae Sheha wa shehia ya Tumbe Mashariki Seif Omar Juma
alisema nivyema kwa kwa halmashauri hiyo kuwaangalia kwa jicho la imani wahanga
hao.
Alisema kuwa kwa kipindi hichi mfuko wa kamati ya maendeleo
ya jimbo la Tumbe ni mdogo sana kwa hivyo wachukuwe hatua za makusudi za kutoa
msaada kwa waathirika waliopatwa na janga hilo .
“Tunaiomba halmashauri hii kwa hali na mali kuweza kutoa
mchango wao ili kuweza kutusaidia kwa hawa walioathirika waliofikwa na janga
hili kutokana na mfuko wetu wa jimbo ni mdogo kwa sasa”,alisema sheha huyo.
Hata hivyo alisema halmashauri hiyo hainabudi kuweza kutoa
mchango wao kwa lengo la kuwasaidia katika shughuli za ujenzi kwa wahanga hao.
Sambamba na hayo alioa wito kwa serikali na wasamaria wema
kuweza kutoa misaada mbali mbali kwa lengo la kuwahami wale wote waliofikwa na
janga hilo .
0 Comments