Habari za Punde

Dk Shein alipokutana na Jumuiya ya wafanyabiashara na wenye viwanda Vietnam

 Baadhi ya Viongozi wa ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakiwa katika mkutano na Jumuiya ya Wafanyabiashara na wenyeviwanda wa Vietnam,wakati wakiwa katika ziara ya Kiserikali nchini humo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa na akizungumza na uongozi wa Jumuiya ya wafanyabiasha,wenyeviwanda na wakulima,katika Mji wa Hanoi Vietnam
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka ya vitega Uchumi ZIPA Salum Khamis Nassor,akitoa mada katika mkutano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na wenyeviwanda wa Vietnam,wakati ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ulipokutana na jumuiya hiyo Mjini Hanoi


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa na akiwapungia mkono wanachama wa Chamber of Commerce and Industry wa nchini Vietnam baada ya kuzungumza nao katika jumba la jumuiya hiyo Mjini Hanoi
 Baadhi ya Mawaziri wa Ujumbe wa Rais wa Zanzibar wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na Mawazori wa SADC,walipofika kumsalimia Rais Dk.Ali Mohamed Shein nchini Vietnam akiwa nchini humo kwa ziara ya kiserikali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Mabalozi  wa Nchi zilizo katika jangwa la Sahara SADC wakati walipofika kumsalimia Rais katika Hoteli ya Melia Mjini Hanoi nchini Vietnam

Picha zote na Ramadhan Othman, Vietnam

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.