Habari za Punde

Said:Nitaibadilisha TOC

 
Na Ameir Khalid
 
MGOMBEA wa nafasi ya urais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Khamis Abdllah
Said, ameahidi kuleta mabadiliko makubwa ndani ya kamati hiyo endapo atashinda katika uchaguzi wa kamati hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Bahari kwenye hoteli
ya Zanzibar Ocean View, Said alisema kuwa ni miaka mingi sasa TOC haijafanya jambo lolote la kujivunia.
Kwa hivyo, amesema ni wazi kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko ili kuona maendeleo ya michezo yanapatikana nchini.
Alisema ushiriki mdogo katika mashindano ya kimataifa pamoja na kukosekana kwa medali kwa wanamichezo wa Tanzania, ni miongoni mwa mambo ambayo wananchi wamechoka nayo.
Mgombea huyo alitaja vipaumbele ambavyo atavifanyia kazi kama atachaguliwa, kuwa rais
wa TOC ni pamoja na kuendesha mambo kisayansi, ikiwa ni kuweka umoja kwa
watendaji, uwazi na uwajibikaji.
Amesema kamwe hatakuwa na tabia ya kuficha mambo, sambamba na kuonesha mshikamano na kuepuka makundi.
Aidha alisema katiba ya TOC inahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa ili kwenda na
Wakati, na kuahidi kulisimamia jambo hilo na kuhakikisha katiba hiyo inapitiwa upya.
Alisema kukosekana ushirikiano kati ya viongozi wa sasa na serikali, ni miongoni mwa kasoro kubwa alizozibaini ndani ya TOC, hivyo atahakikisha anaanzisha tena uhusiano mzuri kati ya pande hizo.
Uchaguzi wa TOC unatarajiwa kufanyika kesho mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.