Habari za Punde

Dk. Shein Afanya Uteuzi

TAARIFA YA UTEUZI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk. Ali Mohamed Shein, amemteua Balozi Isaac Abraham Sepetu kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA).

Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, amesema uteuzi huo umeanza leo Jumatano tarehe 27 Machi, 2013.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

1 comment:

  1. Sijui ni lini Z'bar itapata kiongozi mwenye ujasiri wa kuwaacha viongozi wastaafu kujipumzikia na kuchagua vijana wenye mitazamo mipya?

    Kwa kweli inakera, kila siku majina yale yale ina maana hakuna watu wengine?

    Kama viongozi wastaafu walishaharibu maisha yao, basi waachwe wajutie walichokifanya, hawawezi kubaki madarakani "for ever!

    Sina haja ya kutaja mtu mmoja mmoja lkn. kuna wakuu wa mikoa na wilaya ambao kwa sasa wanastahili kupumzika na wengi wengine ambao wapo kwenye bodi mbali kama vile ZBS(z'bar bureau of std)...kwa kweli msiba huu!

    Hawa watu wakiwa madarakani kazi yao kubwa ni kuoa na kujenga nyumba ktk maeneo yasiyo RASMI ambayo hata kupangisha huwezi..wakistaafu, wanabaki kulia lia!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.