Habari za Punde

Mambo ya Usafiri Huooooooo..........

 Wakati nikiwa katika pirika zangu za hapa na pale kutafuta matukio mitaani nimekutana na Vijana hawa wakiwa katika gari la Punda wakitokea katika maeneo ya Mwanakwerekwe Unguja wakati nikizidi kuzubaa kuangalia huku na kule , na kugunduwa kuwa walikuwa wakirudi mazikoni katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
 Walikwenda mazikoni kumzika kijana mwezao na kupigwa na butwaa huyu marehemu alikuwa katika ajira hii ya kuchukuwa mizigo kupitia gari ya punda au vipi bila kupata majibu ya suala hilo na kuzidi kuona magari ya punda zaidi ya manne yakitokea katika maeneo ya makaburini.
na kurudi mjini baada ya kumalizika maziko hayo na mimi bila ya kupata jibu kulikoni .Mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi marehemu. Amin.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.