Habari za Punde

Vianzio vingi vya maji hatarini kutoweka


Na Mwantanga Ame
KAUKA kwa vianzio vya maji kunakoendelea kujitokeza huenda kukaiweka jamii katika hatari ya kukosa huduma ya maji safi na salama.

Rahika Hamad, mjumbe wa Jumuiya ya Wanamisitu wa Tanzania, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Zanzibar Leo ofisini kwake Maruhubi mjini Zanzibar.

Alisema hali hiyo imeonekana kuongezeka kutokana na vianzio vingi vya maji kuvamiwa na kujengwa makaazi ya watu.

Akitoa mfano alisema ujenzi wa nyumba za makaazi eneo la Welezo na Masingini ambayo ndio roho ya maji, yameathiri kwa kiasi kikubwa upatikanaji huduma ya maji mjini huku baadhi ya mito kama Kitope, Mwera, Bububu, Puu za Saateni, Mtoni, Kinazini na Kitosani ikikauka.


Aidha, alisema hatari zaidi imekuwa ikitengenezwa na wamiliki wa viwanda na baadhi ya watu ambao hutumia eneo la Masingini kumwaga maji ya kemikali zitokazo viwandani na maji machafu kutoka majumbani.

Kutokana na hali hiyo alisema Jumuiya yao imeamua kuanzisha mradi utakaoongeza idadi ya miti katika vianzio vya maji ili kuchangia huduma ya maji.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.