Habari za Punde

Hadithi ya leo (4)


Mtume Muhammad Swalla Allaahu ‘Alayhi wasallam amesema:

للصائم فرحتان فرحة عند فطره، وفرحة عند لقاء ربه " رواه البخاري

Mwenye kufunga huwa na furaha mbili. Furaha ya kwanza wakati anapofuturu na furaha ya pili wakati atakapokutana na Mola wake

Imepokewa na Bukhaari

Furaha hizi zote zina umuhimu wake kwa mja. Anapofutari hufurahi kwa kumaliza kutekeleza agizo la Mola wake alilomtaka afunge. Atakapokutana na Mola wake atakuwa na furaha kwa sababu Allaah Subhaanahu Wata’ala amumuhakikishia kwamba ni  Subhaana mwenyewe ndiye aliyebeba jukuma la kumlipa funga yake.

Ewe Mola tujaalie kuwa miongoni mwa watakaokuwa na furaha hizi huku tukitaka radhi zako.

Aamiyn

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.