Mwandishi wa Raya Hamad akiwazungumza na Waandishi jinsi ya kumsaidia Kijana Haji ambaye amepata ajali ya kuaguka katika Mkarafuu miaka mitatu iliopita na sasa amepata ulemavu, kutokana na ajali hiyo na kuomba Msaada kwa Wasamaria Wema ili kujipatia matibabu. Bi Raya amefanya harambee na kupata kiasi kidogo cha fedha kwa ajili yakupata dawa ambazo anahitaji kutumia kupoza maumivu yake. Kwa wananchi wanaotaka kumsaidia kuwasiliana na Raya Hamad kwa Namba ya Simu 0777 414592. na kwa EmaIl "Raya Hamad"
razildat@yahoo.com, Akiwa na Daftari la dawa la kijana huyu akipiga harambee kwa waandishi wa habari katika Mafunzo ya Kuripoti mazingira magumu, katika harambe hiyo zimepatikana shilingi 50,000/= kwa ajili ya dawa zinazohitajika kupata matibabu yake na kuweza kupatikwa kuweza kununua dawa hizo zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya matibabu yake.
Kijana Haji akiwa Nyumbani kwaoChaani Mkoa wa Kaskazini Unguja, akiendelea na kusubira kupata misaada kwa ajili kupata nafuu ya matatizo yake.
Nawashukuru wadau wote wa Habari kwa kumchango wenu kwa hakika ni wajibu wetu sio ktk kukamata kalamu na kamera lakini penye msaada tunaunaungana pamoja ni vizuri kuzidisha mshikamano wetu na mashirikiano ili kuisaidia jamii , kuibua matatizo yaliyojificha kwa kufuata maadili ya habari ili tusije kuleta migongano pia nachukua fursa hii kuwashukuru wale wote walioupitia ukurasa huu kuusoma nina imani wapo watakaojitokeza kumsaidia kijana huyu kwa kutoa michango yao ama hata ushauri na kwa wale wenye uwezo itakuwa ni vyema kwenda kumuona na kuona hali halisi ilivyo nyumbani kwao CHAANI MCHEZASHAURI au kuwasiliana nae moja kwa moja kwa simu No +255773704853 , Haji Ali Haji alianguka akiwa anaokoa zao la Taifa Karafuu mwaka 2002 wakati akiwa na umri wa miaka 18 hadi leo anashinda na kulala ndani ya kijichumba kidogo chenye mwanga hafifuna hayo ndio mazingira ya hicho kichumba katika picha na kwa bahati mbaya amekosa hisia kuanzia kiunoni kuteremka chini ukweli anahitaji msaada wa hali na mali. AHSANTE.
ReplyDelete