Habari za Punde

Maadhimisho ya Miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwapungia mkono wananchi alipowasili katika viwanja vya Taifa kuhudhuria miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania yaliofanyika katika uwanja huo leo Mjini Dar-es-Salaam.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisimama wakati ukipingwa wimbo wa Taifa alipowasili katika viwanja vya sherehe ya Uhuru leo asubuhi.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua bwaride la Kikosi cha Jeshi la  Wanamaji.
Rais Kikwete akikagua Kikosi cha Jeshi la Anga, wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania. 
Viongozi wa Jukwaa Kuu wakisimama wakati ukipingwa wimbo wa Taifa, katika sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania kutoka kushoto Jaji Mkuu wa Zanzibar,Mhe. Othman Makungu, Makamu wa Rais waJamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Sita Dkt. Amani Abeid Karume na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakihudhuria sherehe hizo katika uwanja wa Taifa Mjini Dar-es-Salaam.

Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, alipowasili jukwaa kuu kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tainzania.







4 comments:

  1. Hakukua na nchi iliyoitwa Tanzania 1961. Wacheni kutuchengua. Simseme tu. Tanganyika.

    ReplyDelete
  2. uhuru wa TANZANIA ! Anavyojuwa Selenunda Tanzania ilianza 1964 na haijawahi kutawaliwa !

    ReplyDelete
  3. " sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tainzania." waandishi tufahamisheni Tanzania ilipata uhuru wake lini na kutoka kwa mkoloni gani please, au mmekusudia uhuru wa Tanganyika nyie?, kama ni hivyo basi msituchezee akili, haya magazeti yanasomwa ulimwengu mzima makosa kama haya mnajirejesha nyuma jamani.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.