Na Hassan Hamad OMKR
Wasomi nchini wametakiwa kuutathmini na kuuchambua mfumo wa elimu iliwa ni pamoja na sera ya elimu ya mwaka 2006, ili kuona iwapo inakidhi matarajio ya sekta ya elimu Zanzibar.
Wito huo umetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akifungua Kongamano la Elimu kuhusu mfumo wa Elimu Zanzibar katika kipindi cha miaka 50 ya Mapinduzi.
Katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka, Mhe. Maalim Seifamesema licha na mafanikio ya kupigiwa mfano katika sekta ya elimu, bado yapo matatizo yanayohitaji kufanyiwa tathmini kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi.
Ametaja baadhi ya matatizo hayo kuwa ni pamoja na upungufu wa vifaa vya kufundishia, ukosefu wa walimu wenye sifa, pamoja na upungufu wa vitabu vya kusomea.
Sambamba na hilo, Maalim Seif amesema mfumo wa elimu uliopo sasa unahitaji kufanyiwa mapitio, ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajiria wapomaliza masomo.
Amewas
isitiza wasomi hao kuendelea kufanya tafiti na kutoa matokeo yake ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayoikabili sekta ya elimu.
isitiza wasomi hao kuendelea kufanya tafiti na kutoa matokeo yake ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayoikabili sekta ya elimu.
Akizungumzia maendeleo ya chuo hicho amesema kimepiga hatua kubwa tangu kilipoanzishwa miaka 15 iliyopita, na kuwataka wanachuo kuongeza juhudi ili kukiletea maendeleo zaidi chuo hicho.
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Iddi Haji Makame amesema tayari chuo hicho kimeanza kutoa shahada za aina nne ikiwemo ya usimamizi wa fedha.
Shahada nyengine wanazotoa ni ICT na uhasibu, manunuzi na usambazaji, pamoja na huduma za benki.
Amesema katika kuhakikisha maendeleo ya chuo hicho wameamua kuwafundisha walimu wao katika ngazi ya udaktari “Phd”, ili waweze kutimiza lengo lao la kuanzisha shahada wa uzamili katika kipindi kifupi kijacho.
Mapema akisoma risala ya ya wanafunzi wa chuo hicho, Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chwaka nd. Shughaib Yussuf Abdi, amesema Mapinduzi ya Zanzibar ni alama isiyoweza kufutika kwa wazanzibari, na kuipongeza serikali ya umoja wa kitafa kwa mafanikio iliyopata
No comments:
Post a Comment