Na Jumbe Ismailly,Singida
DIWANI wa kata ya Unyambwa, manispaa ya Singida, Nd. Shaban Salum na
wenzake, wameburuzwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi mjini hapa,wakikabiliwa na
shitaka la kuchoma moto basi la kampuni ya Mtei Express na kusababisha hasara
ya shilingi milioni 70.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani hapo,
washtakiwa wengine ni Salum Shaban (20), Hashimu Hamisi (20),Hassani Selemani
(54) na Michael Andrew (30).
Wengine ni Ahmed Abdurahmani (24), Yassini Emmanueli (23), Shabani
Hamisi (29), Japheth Eliakimu (38), Ally Mohammedi (29), Ally Japhari (19) na
Shamushidini (32).
Mwendesha mashtaka, Mussa Chemu alidai Januari 9,mwaka huu saa 1:30
asubuhi katika kitongoji cha Ijanuka,kijiji cha Kisasida,washtakiwa wote kwa
pamoja walichoma moto basi la kamapuni ya Mtei Express na hivyo kusababisha
hasara ya shilingi milioni 70.
Mbele ya hakimu, Asha Mwetindwa,washtakiwa hao wote kila mmoja kwa
wakati wake walikana kutenda kosa hilo na kesi hiyo,imeahirishwa hadi Januari
30 mwaka huu itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment