Dk Mohammed Hafidh Khalfan mmoja wa wanabodi wa PBZ alipokuwa akitoa nasaha zake wakati wa ufunguzi wa makao makuu ya Benki ya Kiislamu, Mpirani.
I. Shukran
a. Kwa Allah.
b. Mgeni rasmi
ch. Waalikwa wote na ambao wanafuatilia uzinduzi huu. Kadhalika, waliofanikisha uanzishwaji wa huduma hizi za kifedha kwa mfumo wa Kiislam.
2. Kazi kubwa imefanywa na Serikali yetu ya Zanzibar kuamua kuwa mwanzilishi wa huduma hizi hapa nchini. Inataka ujasiri kutoa huduma mpya ukiwa hujui kama utafanikiwa au laa.
Lilofanywa na SMZ ni kutoa mhanga kitoto chake hicho hicho kimoja kama alivyofanya Nabii Ibrahim 'Alayhis Salaam. kwa mwanawe pekee Ismail 'Alayhis Salaam. Na matokeo ya kuwa tayari kutoa au kufanya kwa ajili ya Aliyetuumba Akaturuzuku ni mafanikio yasiyo shaka. Na tumeanza kuyaona kwa kuongezeka mtaji, idadi ya wateja na kukua uchumi wetu.
Benki ya Kiislam bila ya bima ya Kiislam huwa haijakamilika. Hilo ni ombi letu kwa Serikali yetu sikivu kwa mahitaji ya raiya wake.
3. Nihitimishe kwa kukumbusha kuwa huduma za kifedha zinazofuata Sharia ni nyingi. Nyengine kama vile Sukuk (Islamic Bonds) zimesaidia chumi nyingi duniani hata ambazo wakazi wake wengi si Waislam.
Tusichelewe zaidi, ikiwa Uingereza imejikubalisha kuwa International Islamic Financial Hub kwanini Zanzibar isiwe East African Islamic Financial Hub? Linawezekana pindi tukidhamiria.
Tunaomba katika hili Serikali ikishirikiana na Sekta Binafsi walifanyie kazi kwa dhati na haraka.
Ahsanteni
sijapata kusikia kama kuna bima kama hio , asili ya bima ni wizi uliohalalishwa na serikali kuwanyonya wananchi kwa kupitia mashirika yake ya bima au ya binafsi , na wala hayapo kwa ajili ya kumlinda raia, kwa kifupi tunaomba bima iwe ni jambo la hiari na si lazima kwa sababu hata ukipata ajali bado hulipwi chochote utazungushwaaaaa mpaka uache zana. Tunaomba bima iondolewe ni wiziiiiiiiii , na watu wote wenye kufanya kazi na bima wanajua hilo kuwa wanafanya kazi ktk mashirika ya kijambazi mamboleo, Pato linalopatikana kwa bima ni haramu , kwa hio tusidanganyane kama kuna bima ya halali.
ReplyDelete