Habari za Punde

ZSTC yakabidhi msaada kwa waathirika wa maafa ya moto kisiwani Pemba

 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi, akizungumza na Wahanga waliofikwa na mtihani wa kuunguliwa moto Majumba yao huko katika kiwanja cha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba, kabla ya kupokea msaada ya kutoka ZSTC.


 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi, akipokea Msaada wa Chakula kwa niaba ya Wahanga waliounguliwa moto huko Shehia ya Shumba mjini na Maziwa ng’ombe Wilaya ya Micheweni, kutoka kwa Uongozi wa ZSTC Zanzibar,ukiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo, Mwanahija Almas Ali , huko Micheweni Pemba.

 
Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC Zanzibar, Mwanahija Almas Ali, akizungumza na Wahanga hao huko katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba.

 
Nyumba ambazo tayari zinaendelea kujengwa huko katika Shehia ya Maziwa Ng’ombe huko Micheweni ambazo zinajengwa na Wananchi wenyewe kufuatia kuunguwa kwa moto.

 
Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC, Zanzibar, Mwanahija Almas Ali, akiangalia Nyumba zinazojengwa kufuatia Mtihani huo wa kuunguwa moto huko katika Shehia ya Maziwa Ng’ombe Pemba.

Mkurugenzi Mwezeshaji wa ZSTC Zanzibar ,Mwanahija Almas Ali, akipokea Maelezo juu ya moto ulivyotokezea kutoka kwa Wanakamati ya Maafa ya Shehia ya Maziwa Ng’ombe na jinsi wanavyoendeleza Ujenzi wa Nyumba hizo.
Picha na Bakar Mussa –Zanzibarleo –Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.