Habari za Punde

Makamo wa Rais wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal na Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume Wapiga Kura Yao Skuli ya Kiembesamaki.

 Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume akiwasilikatika viwanja vya Skuli ya Kiembesamaki kupiga kura yake kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki 
 Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume akihakikiwa katika Daftari la WapigaKura  la Jimbo la Kiembesamaki alipofika kituo hapo kupiga kura yake kumchagua Mwakilishi wa Jimbo hilo. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Kituo chake cha kupigia Kura, kwa ajili ya kushiriki kupiga kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki katika uchaguzi mdogo, uliofanyika leo mjini Zanzibar leo asubuhi. Kushoto ni Mgombea wa Jimbo hilo, Mahmoud Thabit Kombo. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimchagua kwa siri mgombea wa Jimbo la Kiembesamaki, katika uchaguzi mdogo wa Mwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika leo mjini Zanzibar. Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitumbukiza  kura yake ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, wakati wa uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo, uliofanyika leo asubuhi mjini Zanzibar. . Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, Mansour Yusuph Himid, kuvuliwa uanachama mwishoni mwa mwaka uliopita

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.