Habari za Punde

Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakipiga Kura Kumchangua Mwakilishi wao.

Mwananchi wa Jimbo la Kiembesamaki akitumia fursa yake kumchagua Mwakilishi amtakae wakati akipiga kura ya kumchagua Mwakilishi wa Jimbohilo katika uchaguzi mdogo unaogfanyika leo katika jimbo hilo.
 Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakiandalia majina yao ili kupata uhakika wa kupiga kura na kujuwa kituo chao cha kupigia kura katika kituo cha skuli ya Kiembesamaki Zanzibar. 
 Afisa wa Tume ya Uchaguzi akimhakiki mpiga kura alipofika katika kituo cha kupiga kura akiangaliwa jina lake katika daftari la wapiga kura.katika kituo hicho.
 Waangalizi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki wakifuatilia upigaji wa kura katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki Msingi, wakiwa katika viwanja vya skuli hiyo.

 Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Ndg. Suluhu Rashid Suluhu, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya zoezi la upigaji kura linavuoendelea katika Jimbo hilo na hakuna fujo wala ucheleweshaji wa kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura na zoezi hilo linakwenda vizuri, katika vituo vyote vya jimbo hilo. 
 Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha ADC, Amani Ismail Rashid, akizungumza na Wapiga kura wake walipofika kupiga kura katika kituo cha Skuli ya Chukwani kupiga kura leo mchana huu. 
 Mgombea Uwakilishi kupitia Chama cha CUF, mHE. Abdulimalik, akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha skuli ya chukwani kuangalia zoezi la upigaji kura linavyoendelea katika kituo hicho. 
 Mgombea wa CUF Mhe. Abdulmalik akitowa malalamiko yake kwa Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar, alipofika katika kituo cha Skuli ya Chukwani kutembelea zoezi hilo la upigaji kura katika kituo hicho.
 Mgombea wa CCM Mhe. Mahmoud Thaib Kombo, akiwasili katika viwanja vya skuli ya chukwani ili kuangalia zoezi hilo na kutumia haki yake kupiga kura katika kituo hicho. ni eneo la makazi yake Chukwani Zanzibar.  
Wagombea wa CCM na CUF, wakisalimiana wakati walipokutana katika kituo hicho wakifuatilia mwenendo wa upigaji wa kura na Mhe. Mahmoud amefika hapo kwa ajili ya kupiga kura yake katika skuli ya Chukwani.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.