Habari za Punde

Mambo ya Maendeleo hayo

Msururo huu wa magari katika barabara ya mlandege wakiwa katika foleni hii kutaka kuingia katika mji mkongwe wa Zanzibar kwa kufuata mahitaji yao na shughuli nyengine za  kijamii. 

2 comments:

  1. Hi ndugu Othman kuwa na magari mengi nchin yaweza kuwa ni maendeleo, lakini kuwa na misusuro mikubwa si dalili ya maendeleo hasa kwa nchi kama Zanzibar bali ni ukosefu wa mipango miji. Hatuna mipango miji Zanzibar. Matokeo yake magari machache tu yanaonekana kusongamano. Hebu tubadilike tuwe serious jamani tuwache siasa chafu tujenge nchi kama wenzetu, au ndo Zanzibar si nchi??
    Wazo langu mimi misururu ya magari inaweza kupungua Zanzibar kwa kutanua huduma mbalimbali za kijamii katika sehemu mbalimbali za mji. Sio kila kitu kuwekwa au kufanywa Darajani, matokeo yake kila mtu ,mwenye gari, pikipiki, baiskeli, gari za punda/ng'ombe na watembea kwa miguu sote hujumuika Dajarani, ambako hakuna plan ya kuhilimi harakati zote hizo za kimaisha.

    Baadhi ya maofisi ya serikali yangehama kule mji mkongwe na kujenga majengo ya kisasa katika maeneo mengine ya mji au nje ya mji kama Mazizini ambapo tayari kumekuwa na mandhari nzuri ya baadhi ya majengo mapya ya ofisi za serikali au taasisi nyengine.

    Masuala ya parking za magari kwetu hatuoni kama ni jambo la maana, matokeo yake magari yana-park barabarani na kuzifanya barabara kuwa finyu mno. Hebu tutenge maeneo ya parking, serikali itakuwa na vyanzo vizuri vya mapato.

    Tuondokane na siasa tuuuuuuuuuu wala sizizo na tija kwa wananchi wa kawaida, kubwa ni kunufaisha wakubwa za familia zao tu, ilhal wanyonge wengi wanateseka na maisha mabovu.

    ReplyDelete
  2. Ipo haja ya kujenga soko kubwa katika maeneo ya chuini kama ilivyo Kwerekwe ili kupunguza msongomano wa watu na magari Darajani.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.