Na Imani Mtumwa. Maelezo. 18.05.2024.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Eliakimu amewataka wananchi kushiriki katika matembezi ya mbio za mwenge ili kutekeleza miradi mbalimbali iliopangwa. Ameyasema hayo huko katika Kiwanja kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru 2024 kutoka Wilaya ya Magharibi B na kukabidhiwa wilaya ya Mjini.
Mzava ameushukuru uongozi wilaya ya magharibi B na Wananchi kwa ujumla kwa mashirikino mazuri waliofanya wakati mwenge wa uhuru ukiwa katika wilaya hiyo jambo ambalo limepelekea mwenge huo kutembezwa kwa vizuri katika maeneo yaliopangwa.
Amesema lengo la mbio za mwenge huo ni kuangalia Maendeleo ya miradi mbali mbali inayotekelezwa sambamba na kujuwa Fedha zilizotumika katika kuimarisha Nchi.
Akizungumza katika zoezi la upandaji wa miti huko kilimani Plaza, kiongozi huyo amewataka viongozi na wananchi kujenga utamaduni wa kupanda miti kwani ni muhimu kwa kuepusha majanga, kuzuia mmongonyoko wa ardhi na kuhifadhi mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mjini Rashid Simai Msaraka amesema Serikali imeweka mikakati mbali mbali ya kuengeza upandaji wa miti ili kuhakikisha wilaya ya mjini inakua na kivutio cha misitu hapa Zanzibar.
“Malengo ya Serikali kupitia mradi huu ni kuhakikisha tunaimarisha mji wa Zanzibar kuwa katika mazingira mazuri na kufikia dhamira ya kuwa kivutio cha Utalii.” alisema Msaraka.
Vile vile amesema kuna miradi mingi ya upandaji miti ili kuepusha majanga yanayoweza kujitokeza ingawa tatizo kubwa ni uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi katika suala la upandaji wa miti.
Jumla ya miradi Nane imetembelewa na kuwekewa jiwe la msingi katika wilaya ya mjini ikiwemo upandaji wa miti kilimani plaza, mradi wa Vijana Mpendae, ujenzi wa maduka skuli ya darajani, kutembelea kituo cha mabasi kijangwani na mradi wa maji safi na salama Saateni ambapo ujumbe wa mbio za mwenge mwaka huu ni "umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa".
No comments:
Post a Comment