Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza katika mkutano wa kampeni na Wananchi wa Kata ya Bwilingu katika Mji wa Mdaula, Msolwa na Chalinze Mzee ikiea ni muendelezo wa kampeni kuomba ridhaa ya wananchi wakichague Chama Cha Mapinduzi ili kiweze kuongoza shughuli za maendeleo katika miaka Mitano inayokuja kuanzia mwaka 2025 hadi 2030.
Nikizungumza na wanachi katika maeneo hayo nimewakumbusha mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 na nia aliyonayo kiongozi wetu kuwa ndiyo msingi mkubwa unaotupa jeuri Cham Cha Mapinduzi. “… katika miaka minne iliyopita Rais Samia ametekeleza ilani kwa ufundi na weledi mkubwa ambalo unampa sifa ya kuwa jemedari bora katika mapambano ya ukombozi wa Watanzania katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii na pia mapambano dhidi ya maadui wakubwa wa nchi yetu.
Nimewakumbusha pia tarehe 29 Oktoba ni siku muhimu kwa wana chalinze kwenda kumshukuru mgombea wa CCM kwa kukichagua chama hiki na wagombea wake kwa kupiga kura nyingi sana na kukipa ushindi mkubwa ili kiunde serikali kwenda kujibu kero au changamoto za wananchi.
No comments:
Post a Comment