Habari za Punde

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiwani Pemba Ndg.Hemed Suleiman Abdulla Akiendelea na Kampeni Jimboni na Kuzungumza na Walimu wa Madrasa

Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiwani Pemba kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na kuomba kura kwa walimu wa madrasa waliomo katika kijiji cha Mauwani Kiwani Pemba.

Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiwani ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema akichaguliwa kuwa mwakilishi wa Jimbo hilo atahakikisha anaipa kipaombele sekta ya elimu ikiwemo kuzisimamia kwa karibu madrasa zote zilizomo jimboni humo. 

Ameyasema hayo wakati akizungumza na kuomba kura kwa walimu wa madrasa zote zilizomo ndani ya jimbo la kiwani. 

Amesema akiwa mwakilishi wa Jimbo la Kiwani kwa kushirikiana na viongozi wenzake atahakikisha analisimamia na kulipa kipaombele kikubwa suala la kuhifadhisha qur-an kwa wanafunzi wote wa jimbo hilo. 

Ndugu  Hemed amasema atahakikisha anaweka mashindano ya qur-an mara mbili kwa mwaka ama  kulingana na makubaliano na walimu na kuahidi kuwa  mwanafunzi atakaetokea wa kwanza anapata zawadi kubwa ambayo inaendana na thamani ya qur-ani. 

Amesema ili mwanafunzi aweze kuhifadhi qur-an ni lazima kuwepo na mazingira mazuri ya kujisomea, kuboreshwa kwa maslahi ya mwalimu pamoja na vifaa vya kusomea na kufundishia hivyo akipata ridhaa ya wanachi ya kuwa mwakilishi wa Jimbo hilo atahakikisha wanafunzi wanahifadhi qur-ani bila ya changamoto yoyote. 

Ndugu Hemed anesema wakati umefika kwa  wanafunzi wa madrasa katika jimbo la kiwani kushiriki katika mashindano ya tahfidhi qur-an sehemu yoyote ile ndani na nje ya Zanzibar bila ya usumbufu wowote. 

Amesema atahakikisha mwalimu wa madrasa wanapata mikopo isiyokuwa na riba ili kuweza kufanya biashara itayomletea kipato cha halali na kuweza kujikimu kimaisha. 

Sambambanna hayo Ndugu Hemed amewataka walimu wa madrasa kutumia elimu zao katika kuwashajihisha vijana juu ya suala la kudumisha amini wakati waote hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. 

Amesema kuwa suala la kutunza amani ni jukumu la kila mmoja wetu pamoja na kuhakikisha amani iliopo nchini inaendelea kudumu sambamba na kutumia fursa hio kuwataka wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 mwezi huu kwenda kuwachagua viongozi ambao watawaletea maendeleo. 

Akizungumza kwa niabaya ya walimu wa madrasa ustadhi Mtumwa Mcha Haji amesema walimu wamadrsa wa jimbo hilo wanakabiliwa na changamoto mbali mbali jambo ambalo linawarejesha nyuma kimaendeleo hasa katika kuhifadhisha qur-an hivyo wamemuomba mgombea huyo kuwatatulia changamoto hizo mara baada ya kumchagua kuwa mwakilishi wao. 

Amesema kuwa viongozi wana wajibu wa kuendeleza masuala ya dini majimboni mwao kwa kuwapatia vifaa vya kufundishia pamoja na walimu kupatiwa mafunzo maalumu ya kufundisha hasa katika tahfidh qur-ani ili kuweza kupata wataalamu wanaokijua vyema kitabu kitukufu cha Qur-an. 

Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe 11 / 10 / 2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.