Habari za Punde

Rais Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Ajumuika na Wananchi Katika Maziko ya Waziri Kiongozi Mstaaf wa Kwanza Zanzibar Marehemu Ramadhan Haji Faki. Yaliofanyika leo 29-3-2020.

Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Waziri Kiongozi wa Kwanza wa Zanzibar na Brigedia Jenerali Mstaaf Ramadhani Haji Faki , wakiingia katika viwanja vya Masjid Mushawar Muembe Shauri Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kuusalimia mwili wa mareheko kwa ajili ya maziko yaliofanyika Kijiji kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 29-3-2020. 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya kumuombea Marehemu Ramadhan Haji Faki Waziri Kiongozi na Bregedia Jeneral Mstaaf, ikiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar. Sheikh. Saleh Omar Kabi, iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja, leo 29-3-2020


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.