Kikosi cha Polisi Wanamaji
Zanzibar kimepokea boti mpya ya kisasa kwa ajili ya shughuli za doria,
operesheni na uokoaji kwenye maeneo ya baharini.
Zoezi hilo la makabidhiano limefanyika leo, Oktoba 8, 2025, ikiwa ni
sehemu ya juhudi za kuimarisha usalama wa watumiaji wa bahari na mali zao.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Wanamaji Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Moshi Sokoro, amesema kuwa, boti hiyo pamoja na nyingine mbili zilizotengwa kwa ajili ya mikoa ya Pemba, zinatarajiwa kuongeza ufanisi wa Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani na usalama kwenye maeneo ya bahari.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Christopher Fuime, ambaye amepokea boti hiyo kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, amesema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Taasisi na Wadau wengine kuhakikisha boti hizo zinatumika ipasavyo katika kukabiliana na vitendo vya kihalifu baharini.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Bandari Zanzibar, Bw. Akif Ali Khamis, amepongeza hatua hiyo na kueleza
kuwa, uwepo wa boti hizo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha ulinzi
na usalama katika maeneo ya bandari na maeneo ya mwambao kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment