Habari za Punde

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA UAPISHO WA RAIS WA MALAWI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Getrude Mutharika, Mke wa Rais wa Malawi, Profesa Arthur Mutharika  alipomwakilisaha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uapisho wa Rais huyo uliofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu, Blantyre nchini humo  Oktoba 4, 2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Rais wa Malawi na Jaji Mstaafu  Dkt.  Jane Ansah alipomwakilisaha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uapisho wa Rais mteule wa Malawi, Profesa.  Arthur. Mutharika uliofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu,   Oktoba4, 2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Rais wa Msumbiji, Daniel Chapo alipomwakilisaha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uapisho wa Rais mteule wa Malawi, Profesa.  Arthur. Mutharika uliofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu uliopo Blantyre,  Oktoba4, 2025.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Rais wa Malawi Prof. Arther Mutharika katika sherehe za kumuapisha Rais huyo zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu, Blantyre nchini humo Oktoba 04, 2025. Kulia ni mkewe Getrude Mutharika. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe hizo 

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Rais wa Malawi Prof. Arther Mutharika ujumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipomwakilisha Rais Dkt. Samia katika sherehe za kumuapisha Rais wa Malawi, kwenye uwanja wa Kamuzu, Blantyre nchini humo Oktoba 04, 2025.
Rais wa Malawi Profesa Arthur Mutharika akizungumza baada ya kuapishwa kwenye Uwanja wa Kamuzu uliopo Blantyre nchini Malawi, Oktoba 4, 2025. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho huo.
Rais  Mstaafu wa Malawi, Bakili Muluzi alikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika Uapisho wa Rais mteule wa Malawi, Profesa.  Arthur. Mutharika kwenye uwanja wa Kamuzu,   Oktoba4, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho huo.
Rais wa zamani wa Malawi, Joyce Banda alikuwa miongoni mwa washiriki wa sherehe za Uapisho wa Rais mteule wa Malawi, Profesa.  Arthur. Mutharika uliofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu uliopo Blantyre, Oktoba 4, 2025.. Waziri Mkuu, Kassim Majliwa alimwakilisha Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan katika sherehe hizo,    Oktoba4, 2025.
Mmoja wa washiriki wa sherehe za Uapisho wa Rais mteule wa Malawi, Profesa.  Arthur. Mutharika akifuatilia sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu, uliopo Blantyre nchini Malawi    Oktoba4, 2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.