Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni mgombea wa uwakilishi Jimbo la kiwani Pemba ndugu Hemed Suleiman Abdulla katika Mkutano ufunguzi wa kampeni za CCM Jimbo la Welezo uliofanyika katika Uwanja wa Stella Darajabovu Wilaya ya Magharibi “ A “ Unguja.
Amesema ndani ya Jimbo la Welezo serikali imejenga barabara ya Mkapa Road inayotoka Amani hadi Mtoni pamoja na kukamilisha ujenzi wa daraja katika barabara hio.
Kwa upande wa barabara za ndani zilizomo katika Jimbo la Welezo tayari zimeshafanyiwa upembuzi yakinifu na ujenzi wake unatarajiwa kuanza wakati wowote.
Akizungumzia ujenzi wa miundombinu ya skuli Mhe.Hemed amesema katika Jimbo la Welezo imejengwa skuli ya Sekondari ya Hassan Khamis Hafidh ya ghorofa ya (G+3), Skuli ya Msingi Mtofaani imekamilika ambapo ujenzi wa skuli ya Msingi Mtopepo ya (G+2) unaendelea na hatua za awali za ujenzi wa wa skuli ya Sekondari Mtofaani (G+3) zimekamilia na ujenzi wa skuli hio wakati wowote utaendelea.
Akizungumzia Sekta ya Afya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefahamisha kuwa ujenzi wa hospitali ya Jeshini Welezo unaendela na ikikamilika itatoa huduma mbali mbali kwa wananchi ikiwemo huduma za uzazi salama.
Aidha, Mhe. Hemed amesema ujenzi wa soko la Makufuli umekamilika na linaendelea kutumika ambapo ujenzi wa nyumba za wazee za kisasa Welezo unaendelea na utakapokamilika utatoa fursa kwa wazee kuishi katika makaazi bora na salama.
Sambamba na hayo, Mhe. Hemed ametoa nasaha kwa wananchi kuendelea kudumisha amani kwa kutokubali kutumika kuvuruga amani iliyopo nchini pamoja na kujitokeza kwa wingi katika kukipigia kura chama cha Mapinduzi (CCM ) ifikapo Oktoba 29, 2025.
Amewakumbusha wagombea wa CCM kufanya kampeni za kistaarabu na kutokubali kuchokozeka katika kipindi chote cha kampeni na kuwataka wagombea hao kuyatumia majukwaa ya kampeni kwa kuinadi Ilani ya CCM pamoja na kuwaeleza wananchi mazuri yote yaliyofanywa na maraisi Wote wawili.
Mhe.Hemed ametumia Mkutano huo kuwanadi na kuwaombea kura wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Jimbo la Welezo pamoja na kuwataka wanachi kuwachagua wagombea wote wa chama cha mapinduzi ili waweze kuwasaidia vyema katika kuleta maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya wagombea wenzake Mgombea Uwakilishi Jimbo la Welezo Ndugu Mhe. Hassan Khamis Hafidh akizungumza kwa niaba ya wagombea wenzake amesema watashirikiana kwa pamoja na viongozi wenzake kuhakikisha jimbo la Welezo linaendelea kupiga hatua kimaendeleo katika sekta zote za Kimkakati.
Ndugu Hafidh amesema anatambua changamoto ndogo ndogo zilizomo ndani ya Jimbo la Welezo hivyo watakapowachagua na kuwa viongozi wa Jimbo hilo wanawaahidi wanawelezo kuzifanyia kazi na kuziondoa changamoto hizo kwa ustawi bora wa jimbo hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi kichama ndugu Mohammed Rajab Soud ameitumia hadhara hio kuwaombea kura wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya Uraisi hadi usiwani ili waweze kushinda na kuendeleza yale mazuri wanauoendelea kuyafanya nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )
Leo tarehe 03 / 10 / 2025
No comments:
Post a Comment