Habari za Punde

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2025 Matukio ya Picha Kutoka Zanzibar

Kamishna wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi ya Zanzibar, Khatib Mwinyichande (wa pili kulia) akizungumza kwenye kikao cha pamoja baina ya tume hiyo na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC kilichofanyika ofisi za INEC zilizopo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni utaratibu wa THBUB kukutana na wadau wa Uchaguzi wakiwa kwenye mwendelezo wa Uangalizi kuelekea Uchaguzi mkuu 2025 wakati wa kampeni kwa vyama mbalimbali vya siasa. Wa kwanza (kulia) ni Mratibu wa Uchaguzi Unguja (REC) Bw. Abdallah Bakar Khamis, Katibu Msaidizi THBUB Bw. Juma Msafiri Karibona (katikati), Bw. Wilfred Msagati Afisa Sheria, THBUB Unguja (wa pili kushoto) na Bitizani Kejo, Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka THBUB Dar es Salaam.

.  Kamishna wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi ya Zanzibar, Khatibu Mwinyichande (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa tume hiyo pamoja na maofisa wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC mara baada ya kikao cha pamoja kilichofanywa na tume mbili hizo kwenye ofisi za INEC zilizopo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni utaratibu wa THBUB kukutana na wadau wa Uchaguzi wakiwa katika mwendelezo wa Uangalizi kuelekea Uchaguzi mkuu 2025 wakati huu wa kampeni zinazoendelea kwa vyama vya mbalimbali vya siasa.

1  Timu ya maofisa wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wakiwa kwenye mwendelezo wa kukutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi vikiwemo vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2025. Pichani ni Maofisa wa THBUB (kushoto) wakiwa kwenye kikao cha pamoja na wanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo (kulia) ofisi za ACT, Vuga Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, hivi karibuni.

1.    Maofisa kutoka Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), (kulia) wakizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Taifa (AAFP), ambae pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho, Bw. Said Soud Said huko ofisi za Chama hicho Mwera, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi. THBUB inafanya mwendelezo wa kuwatembelea wadau wa uchaguzi zikiwemo Tume za Uchaguzi za ZEC na INEC, vyama vyote vya siasa wakiwemo viongozi na wadau wa vyama hivyo, THBUB inafanya zoezi maalumu la uangalizi wa uchaguzi kuelekea Uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, 2025.

Maofisa kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mafunzo ya Haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kisiwani Pemba, kuelekea Uchaguzi mkuu Oktoba 2025, waliokaa katikati ni Kamishna wa (THBUB) ofisi ya Zanzibar, Khatib Mwinyichande, Afisa Mfawidhi THBUB kituo cha Pemba Bw. Suleiman Salim (kulia) na Mratibu kutoka Idara ya Habari Maelezo ofisi ya Pemba, Bi. Jamila Abdallah Salim (wa Kwanza kushoto). Mafunzo hayo yalifanyika hivi katika ofisi za THBUB zilizopo Mtaa wa Kichungwani, Wilaya ya Chachake, Mkoa wa Kusini Pemba. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.