Habari za Punde

Mgombea Ubunge Kwa Tiketi ya CCM Jimbo la Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete Akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni Kata ya Msata na Kiwangwa

Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete akiendelea na mikutano yake ya kampeni ya hadhara na ya ndani kuzungumza na Wananchi kuinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2025, kuomba kura na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Wabunge wote wa CCM na Madiwani.  

Wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Msata na Kiwangwa katika vikao vya ndani kuendelea kuomba kuungwa mkono ili kushinda katika uchaguzi mkuu 29,oktoba 2025. 

Na kukumbushana wajibu wetu kama Viongoz wa Chama cha Mapinduzi na pia kukumbusha yale mahsusi ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025 katika maeneo yetu. Viongozi na wananchi wameendelea kuelimika na Kazi inaendelea. 



Wananchi wa Kata ya Msata na Kiwangwa Jimbo la Chalinze wakiwa katika  mkutano wa ndani wakimshangilia mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze wakati akizungumza na kuinadi Ilani ya Uchaguzi wa CCM Mwaka 2025.  



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.