Habari za Punde

Kasesela Awahamasisha Watanzania Kumuabudu Mungu na Kupiga Kura

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) na Mratibu wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanda ya Dar es Salaam, Richard Kasesela, amewataka Watanzania kumuabudu Mwenyezi Mungu kila wakati ili waweze kupata amani ya moyo na nafsi.

Baadhi ya waumini wa dini ya wananchi waliohudhuria kongamano la waislamu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu lilofanyika mlimani city jijini Dar es salaam.

Baadhi ya waumini wa dini ya wananchi waliohudhuria kongamano la waislamu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu lilofanyika mlimani city jijini Dar es salaam

Na Fredy Mgunda 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) na Mratibu wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanda ya Dar es Salaam, Richard Kasesela, amewataka Watanzania kumuabudu Mwenyezi Mungu kila wakati ili waweze kupata amani ya moyo na nafsi.

Akizungumza katika kongamano la Waislamu kuelekea uchaguzi mkuu, Kasesela alisema ni muhimu kwa wananchi kusoma vitabu vya dini mara kwa mara, kwani vinafundisha maadili mema na kuleta baraka katika kazi zao za kila siku.

"Vitabu vya dini vinatufundisha subira, heshima na upendo – misingi ambayo ni muhimu katika maisha na maendeleo ya taifa," alisema Kasesela.

Aidha, aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu ya kiroho sambamba na mafunzo ya mbinu za kujikwamua kiuchumi, ili wananchi waweze kujitegemea na kuboresha maisha yao.

Katika hatua nyingine, Kasesela aliwahimiza wananchi wote kumpigia kura kwa wingi Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa amefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika kipindi chake cha uongozi.

"Ni wajibu wetu kuonyesha shukrani kwa kumpigia kura Dkt. Samia tarehe 29 Oktoba. Tuonyeshe mshikamano wetu kwa kupitia sanduku la kura," alihitimisha Kasesela.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.