Mhe. Mwinyichande alitoa
nasaha hizo jana ofisini kwao Mombasa Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini
Magharibi kupitia semina ya wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) waliopewa watumishi wa tume hiyo.
Aidha aliwasihi watumishi hao
kujiunga na mfuko huo kwani ni mzuri na una faida kwao na kwa familia zao,
akilisifia ‘fao la kifo’ ambalo litamnufaisha mtumishi wa mfuko huo hata baada
ya kuondoka duniani.
Naye, Katibu Msaidizi THBUB,
Bw. Juma Msafiri Karibona aliishukuru PSSSF kwa ushirikiano wanaoutoa kwa
watumishi wa umma sambamba na kuwaomba kuwafikia watumishi wa THBUB kisiwani
Pemba.
Mapema, akichambua mada ya ‘fao la kifo’, mbali na mafao mengine
aliyoyajadili kwenye semina hiyo, yakiwemo mafao ya uzazi, uzee, ulemavu, kukosa
ajira, ugonjwa na fao la wategemezi, Afisa
huduma kwa wateja wa mfuko wa PSSSF, Ndg. Marry Malilo amesema, Mtumishi wa
umma akiwa mwanachama wa mfuko huo endapo atafariki watamchangia marehemu shilingi
laki tano kwenye mazishi yake, mbali na kutoa mafao mengine ya urithi kwa warithi
halali wa marehemu pia mfuko utaendelea kuwalipa mpencheni ‘Mjane’ au ‘Mgane’
wa marehemu pamoja na watoto wa marehemu walio chini ya umri wa miaka 18 kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo na watalipwa kima cha mshahara aliokua
akiupokea marehemu.
Kwa uapande wake Mwezeshaji wa
Mfuko huo, Bw. Seif Khamis Moh'd wakati akitoa elimu ya Mfuko huo kwa Watumishi
wa THBUB kupitia Semina ya wanachama wa mfuko huo, aliwashauri kujipanga mapema
kimaendeleo kabla ya kusubiri kustaafu.
Aliwahimiza watumishi hao kupitia
mada ya ‘kustaafu’ aliwasihi kujiandaa mapema kwa kijiwekea akiba mapema ili
kujijengea mazingira nazuri watapo staafu.
Aidha, aliwashauri watumishi hao
kuanza mapema kujiekeza kwenye uchumi kwa kujiwekeza mapema kabla ya kustaafu
kwao.
Hata, hivyo aliwasihi
watumishi hao kujiepusha na maisha ya anasa na ya fahari kubwa kwa kipindi
chote cha utumishi wao ili wapate nafasi ya kujiwekea akiba endapo watafikia
mwisho wa utumishi wao (kustaafu).
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ulianzishwa mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment