Habari za Punde

Mkutano wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Kwahani Viwanja Vya Farasi Kwahani Wilaya ya Mjini Unguja

Mgombea Ubunge Jimbo la Kwahani Zanzibar Mohammed Laki  akicheza mziki wa singili wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Jumbo la Kwahani uliyofanyika viwanja vya farasi Kwahani Wilaya ya Mjini Unguja. 

Wagombea Ubunge na Uwakilishi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kwahani Zanzibar (kushoto) Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kwahani Mhe.Mohammed Sijaamini na (kulia) Mgombea Ubunge Jimbo la Kwahani Mhe.Mohammed Abdalla (Laki) , wakibadilishana mawazo wakati wa mkutano wao wa Kampeni uliyofanyika viwanja vya farasi Kwahani.

Mwenyekiti wa Jimbo la Kwahani Mhe.Khamis Yussuf Mussa (Pele) akizungumza na kumkaribisha mgeni rasmin kuzungumza na kunadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2025 na kuwaombea Kura wagombea , wakati wa mkutano wa kampeni uliyofanyika katika viwanja vya farasi kwahani Wilaya ya Mjini Unguja.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Ndg.Hussein Ayoub Iddi akizungumza wakati wa mkutano wa Kampeni ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Kwahani Zanzibar, uliyofanyika katika viwanja vya Farasi Kwahani na kuinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025 na kuwaombea Kura Wagombea ya CCM wote.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Ndg.Hussein Ayoub Iddi akiwatambulisha Wagombea Ubenge na Uwakilishi wa Jimbo la Kwahani Zanzibar, wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Farasi Kwani Wilaya ya Mjini Unguja na (kulia kwake) Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kwahani Mohammed Sijaamini (kushoto kwake) Mgombea Ubunge Jimbo la Kwahani Mohammed Abdallah(Laki) 




















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.