Habari za Punde

Maalim Seif afutarisha

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitoa nasaha zake baada ya kujumuika na wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani katika futari ya pamoja aliyoindaa kwa ajili ya wanachuo hao.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani Dr. Hamed Rashid Hikman, akitoa neno la shukrani kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kujumuika na wanafunzi wa Chuo hicho katika futari ya pamoja
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na viongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani, alipowasili chuoni hapo kwa ajili ya futari ya pamoja na wanachuo hao.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani wakijumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad. (Picha na Salmin Said, OMKR).
 
Na: Hassan Hamad (OMKR).
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amejumuika pamoja na wanafunzi na watendaji wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani katika futari ya pamoja, na kutaka utamaduni wa kufutarishana miongoni mwa waislamu uendelelezwe.
 
Amesema utamaduni huo ni muhimu na utapaswa kuendelezwa kwa vile unajenga mapenzi, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu, na kwamba hatua hiyo itavirithisha vizazi vijavyo utamaduni ulio bora.
 
Maalim Seif amewashukuru wanachuo hao kwa kukubali kujumuika nao katika futari hiyo ya pamoja, na kuwatakia kheri ya mfungo mtukufu wa Ramadhani.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dr. Hamed Rashid Hikman amemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuamua kujumuika na wanachuo katika futari hiyo ya pamoja.
 
Dr. Hikman amesema kitendo cha viongozi kujumuika pamoja na wananchi  katika shughuli za kijamii ikiwemo futari, ni jambo la msingi ambalo linajenga umoja na upendo  kati ya wananchi na viongozi.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameanza kuwafutarisha wanachuo hao, ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kufutarisha makundi mbali mbali ya kijamii yakiwemo ya wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi mbali mbali kupitia ngazi za Wilaya na vijiji, kila ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.