Habari za Punde

Shamrashamra za wiki ya maji zikiendelea kisiwani Pemba

 MKUU wa Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba Mhe:Hemed Suliman Abdalla, akikunjuwa kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la kisima cha Maji safi na salama huko Mahuduthi, ikiwa ni shamra shamra za wiki ya maji duniani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akizunguma na wananchi wa Mahuduthi wilaya ya Mkoani mara baada ya kuweka jiwe la msingi kisima cha Maji safi na salama huko Mahuduthi.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Wilaya ya Wete Mkao wa Kaskazini Pemba Mhe:Hassan Khatib Hassan, akikunjuwa kitambaa kuashiria uzinduzi wa maji katika kijiji cha Chekea jimbo la Mtambwe, ikiwa ni shamra shamra za wiki ya maji duniani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Wilaya ya Wete Mkao wa Kaskazini Pemba Mhe:Hassan Khatib Hassan, akifungua mfereji kuashiria utokaji wa maji mara baada ya kuuzindua rasmi maradi huo, huko katika kijiji cha Chekea jimbo la Mtambwe, ikiwa ni shamra shamra za wiki ya maji duniani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WASOMAJI utenzi maarufu kisiwani Pemba, Fatma na Farhia wakighani utenzi huo huko katika kjiji cha Chekea Mtambwe katika uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ikiwa ni wiki ya maji duniani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Wilaya ya Wete kisiwani Pemba, Mhe:Hassan Khatib Hassan akizungumzia na wananchi wa Chekea Mtambwe, mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama kijijini hapo. .(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.