Habari za Punde

Wanafunzi wa Tanzania Wanaosoma Mjini Beijing China

Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Tanzania Wanaosioma Mjini Beijing Ndg Suleiman Serera , akiagwa na Mtaalamu wa IT wa Jumuiya hiyo Ndg Salum Ramadhani baada ya kuchaguliwa mwenyekiti mpya katika Mkutano Mkuu huo uliofanyika Chuoni hapo.

Katika Uchaguzi huo Mkuu wa Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Mjini Beijing China, 
Wamemchagua Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kura nyingi Ndg Ireneus Kagashe  na Makamo Mwenyekiti Ndg Mara Abdurahaman Said kwa upande wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo amechaguliawa Ndg. Godfrey Steven na nafasi ya Naibu Katibu Mkuu imechukuliwa na Ndg Asha Hijja kwa upande wa Mtunza Hazina (Fedha) Ndg Ezekiel Elineema.  
 Balozi wa Tanzania Nchini China Balozi Abdurahaman Shimbo(katikati) akifungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi Watanzania wanaosoma Mjini Beijing China, uliofunguliwa na Balozi Shimbo.  kushoto Muambata wa Ubalozi wa Tanzania Elimu George Manongina kulia Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Wanafunzi  wanaosoma Mjini Beijing China Ndg Suleiman Serera  
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaosoma Beijing wakimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini China akifungua Mkutano wao Mkuu wa kuwachagua Viongozi wapya kwa mwaka 2015/2016 
Mmoja wa Mwanafunzi akiuliza swali wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika Mjini Beijing China, Mkutano huu umewajumuisha Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Beijing Tu.

Napiga Kura yangu kumchagua nimtakae natimiza demokrasia yangu ya kumchangua nimtakae.
                  Wanafunzi wakipiga kura yao kuwachagua viongozi wa jumuiya yao.
                                                                   Wakipiga kura yao
Akiwa na tabasamu wakati akipiga kura yake kumchagua Viongozi wao wa Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma Beijing China.  
Wanafunzo wa Kitanzania wanaosoma Beijing wakiwa na tabasamu kumpigia Kiongozi wa Jumuiya yao na kutumia Demokrasia yao kumchagua wamtakae
Wakihakikisha kura yao haiharibiki wanaitumia vilivyo kumpata Kiongozi Bora kuwaongoza kwa mwaka wa masomo 2015/2016
 Wakati wa kuhesabu kura umefika na zoezi hilo kuaza kuwapata washindi wa Uchaguzi huo Mkuu.
Zoezi likiendelea la kuhesabu kura kama wanavyoonekana Kamati ya Uchaguzi ikifanya kazi yake. ya kuhesabu kura. 
Zoezi likiendelea la kuhesabu kura kama wanavyoonekana Kamati ya Uchaguzi ikifanya kazi yake. ya kuhesabu kura.
Balozi Abdurahaman Shimbo akiondoka katika ukumbi wa mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Tanzania Wanaosoma Beijing China, akiongozania na Mtaalam wa IT wa Jumuiya hiyo Ndg Salum Ramadhan.  
to: MUHIDIN MICHUZI , Othman Michuzi cc: sek david , Francis Dande , GSengo , Omar Fungo , Gadiola Emanuel , Francis Godwin , Haki Ngowi , Jestina George , Kambi Mbwana , Josephat Lukaza , "Mhamila .Rajabu" , Henry Mdimu , Exaud Mtei , Maggid Mjengwa , Emmanuel Shilatu , Ester Ulaya , Uwazi Publishers , Robert Okanda , Geofrey Adroph , "woindeshizza@yahoo.com" , Dotto Mwaibale , RAHEL PALLANGYO , John Bukuku , Jane John , "mushi@thehabari.com" , zainul mzige , william malecela , Jeff Msangi , linda shebby , Mroki Mroki , Shebby Mpondela , Bashir Nkoromo , bertha ismail , Mbeya Yetu yle="clear: both; text-align: center;">
Viongozi Wapya waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni kumbukumbu ya Uchaguzi huo.
Viongozi Wapya waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja ikiwa ni kumbukumbu ya Uchaguzi huo.
Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Beijing China wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo na kuwapata Viongozi wapya baada ya kuchagulia kwa kuongoza Jumuiya hiyo kwa mwaka 2015/2016

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.