Habari za Punde

Balozi Seif akiongoza Kikao cha dharura cha Kamati ya Taifa ya kukabiliana na maafa

 Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya kukabiliana na Maafa Zanzibar ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mzee  Salhina Abdi Mkufau wa Shehia ya Jang’ombe ambye nyumba yake imebomoka baada ya kuzibuka kwa shimo kubwa pembezoni mwa kuta ya nyumba hiyo.

Nyuma ya Balozi Seif  ni Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe Mheshimiwa Salum Suleiman Nyanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr. Salem Mohammed Jidawi akisisitiza umuhimu wa Jamii kuimarisha huduma za Afya ili kujiepsha na miripuko ya maradhi katika Kikao cha dharura cha Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar kilichokutana Ofisini mwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

Wa kwanza kulia ni Waziri wa Kilimo Dr. Sira Ubwa, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman, Waziri wa Afya Mh. Rashid Seif, Waziri wa Nchi Ikulu na Utawala Bora Dr. Mwinyihaji Makame, Kamishana wa Polisi Zanzibar CP Hamdani Mohammed, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid.
Balozi Seif akikiongoza Kikao cha dharura cha Kamati ya Taifa ya kukabiliana na maafa Zanzibar kilichokutana ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kuthathmini athari ya mvua zilizoleta maafa Zanzibar.

Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d, Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano Mh. Juma Duni Haji,Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Dr. Idriss Muslim Hijja, Waziri wa Habari, Mh. Said Ali Mbarouk, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omar Kheir na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Ujenzi Mhandisi Ramadhan Mussa Bakari akizitaja baadhi ya matatizo yanayochangia kuibuka kwa maafa nchini zinazosababishwa na wanaadamu kwenye kikao cha dharura cha Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar.

Picha na –OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.