Habari za Punde

Maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mjini Abijah - Ivory Coast

  Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika,Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali akiteta jambo na Mawaziri wa Fedha mbalimbali waliohudhuria mkutano huo  Mjini Abijah-Ivory coast.
Baadhi ya Marais wa Afrika waliohudhuria mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mjini Abijah-Ivory coast.

Rais wa Benki wa Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka akiwa kwenye kikao na Magavana wa Afrika wakijadiliana changamoto mbalimbali za maendeleo zilizojitoketeza katika nchi za Afrika Mjini Abijah- Ivory coast.
 Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali akisikiliza majadiliano kwenye kikao cha magava wa nchi za Afrika wakati wa kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo Mjini Abijah-Ivory.

 
 Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicus B.Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa majadiliano pamoja na Mkurugenzi Mkuu Bw. Gabrriel Negatu  wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Abijah-Ivory coast
 Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji akitoa ufafanuzi kwa Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Ngosha Magonya akiwa pamoja na Afisa Mwandamizi  Bw. John L. Sima Mjini Abijah-Ivory Coast.
Kamisha wa Fedha za Nje wa Zanzibar Bi. Bihindi N.Khatibu akiwa kwenye mkutano siku ya kufunga kwa mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)Mjini Abidjan-Ivory Coast



Rais Mpya wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akihutubia na kutoa shukrani kwa wajumbe kwa kuchanguliwa kuwa rais wa benki hiyo Mjini Abidjan-Ivory Coast.

Rais Mpya wa Benki wa Maendeleo ya Afrika(AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akiwa pamoja na baadhi ya marais kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB) Mjini Abidjan-Ivory Coast.(Picha zote na Scola Malinga-Abidjan).


1 comment:

  1. Maelezo hayaendani na picha..Gavana Ndullu hayupo pichani kama unavyoeleza!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.