Habari za Punde

Waziri Mwandyosa Ahudhuria Hafla ya Kukabidhi zawadi Wanafunzi wa Michipuo Pemba.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe:Profesa Mark Mwandosya, akizungumza na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Vijana Ndg.Daudi Khamis Juma, wakati alipowasili katika skuli ya Wawi Msingi Chake Chake Pemba, katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi 17 waliopasi Michipuo mwaka 2014/2015
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi wa wanafunzi wa skuli ya Wawi msingi Chake Chake Pemba, katika hafla ya kuwakabidhi zawadi wanafunzi 17 waliofaulu Michipua.  
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe:Profesa Mark Mwandosya, akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi wa Skuli ya Wawi Msingi Kisiwani Pemba, kabla ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi 17 waliofaulu Michipuo wa Darasa la Saba mwaka 2014/2015
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe:Profesa Mark Mwandosya, akimkabidhi Zawadi mmoja kati ya wanafunzi 17 waliofaulu Michipuo katika Skuli ya Wawi Msingi Kisiwani Pemba, ikiwa ni ahadi iliyotolewa na kada wa Chama cha Mapinduzi kupitia NEC Vijana Ndg.Daudi Khamis Juma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalumu Mhe:Profesa Mark Mwandosya, akipokea viatu vya makubazi kutoka kwa uongozi wa skuli ya Wawi Msingi Kisiwani Pemba, ikiwa ni miongoni mwa zawadi alizopatiwa na uongozi wa skuli hiyo
Waziri wa Nnchi Ofisi ya Rais Kazi Maalumu Mhe:Profesa Mark Mwandosya, akipokea zawadi ya ndizi ya Mkono mmoja kutoka kwa Mwenyekiti wa Skuli hiyo Nassor Mohamed Ibrahim.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.