Habari za Punde

Michuano ya Kombe Mapinduzi Jamuhuri na URA Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya URA imeshinda bao 1--0.

 
 Makamu mwenyekiti wa Baraza la Machezo Zanzibar Khamis akisalimiana na Waamuzi wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi kati ya Timu ya Jamuhuri na URA mchezo uliofanyika jioni hii. Katika mchezo huo Timu ya URA imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe kla Mapinduzi kwa kuifunga timu ya Jamuhuri kwa Bao 1--0 , wakati wa mchezo wao wa mwisho uliofanyika jioni hii Ikisubiri hatma ya Timu ya Simba na JKU zinazocheza usiku huu kila moja ikiwa na tamaa ya kuungana na URA. Timu ya Simba ikiwa na point 4 na Timu ya Jamuhuri ikiwa na pointi 3.
 Waamuzi wa mchezo wa URA na JKU wakiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa JKU na URA kabla ya kuaza kwa mchezo huo uliofanyika jioni hii uwanja wa Amaan Zanzibar .
Kikosi cha Timu ya Jamuhuri Kilichoshiriki Kombe la Mapinduzi kilichokubali kipigo cha bao 1--0 jioni hii
Kikosi cha Timu ya URA kutoka Nchini Uganda kilichofanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Timu ya Jamuhuri katika mchezo wao wa mwisho kwa bao 1--0.
Beki wa timu ya URA Senkoomi Sam akiwa hewa akipiga mpira wa kichwa huku mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri Khamis Hamad akijaribu kupapatua mpira huo bila ya mafanikio.
Mshambuliaji wa Timu ya Jamuhuri Khamis Hamad, akijaribu kumpita beki wa timu ya URA Senkoomi Sam wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi timu ya URA imeshinda bao moja 
1--0
Beki wa Timu ya URA Allan Munaaba  na mshambuliaji wa timu ya Jamuhuri Mwalim Khalfan wakiwania mpira wa juu wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mchezaji wa Timu ya Jamuhuri na URA wakiwania mpira. 
 Beki wa Timu ya URA  Kyeyune Saio akiondoa mpira wakati wa mchezo wao wa mwisho wa kombe la mapinduzi huku mshambuliaji wa timu ya jamuhuri Bakari Futo, katika mchezo huo timu ya URA imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi ikisubiri mchezo wa JKU na Simba ili timu moja iungane nayo katika michezo ya Nusu Fainali na Timu za Yanga na Mtibwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.