Habari za Punde

KAMPUNI YA UDALALI YAVUNJA NYUMBA SHEKILANGO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Kijiko cha Kampuni ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd kikibomoa nyumba za makazi ya watu na biashara zilizojengwa katika eneo la Kampuni ya Dar es Salaam Cold Makers Ltd lililopo Shekilango Sinza jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwananchi akiangalia mabaki ya nyumba zilizobomolewa katika eneo hilo.



 Kijiko kikibomowa moja ya baa zilizokuwepo eneo hilo jirani na Baa ya Rego iliyopo Sinza jijini Dar.
 Wananchi, wamiliki wa nyumba na mabaa katika eneo wakiwa wamepigwa butwaa
 Mabati yakiondolewa eneo hilo.
 Hapa ni kupiga picha eneo la tukio na huzuni tupu.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio.
 Kijiko kikibomoa nyumba ya ghorofa katika eneo hilo.
 Askari Polisi na mgambo wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi.
Kontena likiondolewa katika eneo hilo inadaiwa mmiliki wa kontenta hilo aliuziwa eneo hilo miezi ya hivi karibuni kwa sh.milioni 400. hakika ni hasara kubwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd imebomoa nyumba za makazi ya watu na biashara zilizojengwa katika eneo la Kampuni ya Dar es Salaam Cold Makers Ltd lililopo Shekilango Zinza jijini Dar es Salaam.

Uvunjaji wa nyumba hizo uliofanyika Dar es Salaam leo ambao ulisimamiwa na jeshi la polisi na mgambo uliwaanja mdomo wazi na wasijue cha kufanya wamiliki wa nyumba hizo na wafanyabiashara wa nyama choma ya nguruwe ambao wengi wao walishindwa kuondoa mali zao na kujikuta wakiingia hasara kubwa.

Akizungumza na wanahabari eneo la tukio Meneja wa Biashara wa kampuni hiyo ya udalali, Elieza Mbwambo alisema wamebomoa nyumba hilo kwa agizo la mahakama baada ya mteja wao Dar es Salaam Cold Makers kushinda kesi ya msingi iliyofunguliwa na mtu aliyetajwa kwa jina la Ondolo Chacha aliyekuwa akidai eneo hilo ni lake.

Mbwambo alisema kuwa eneo hilo lililokuwa linadaiwa kuwa ni mali ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kampuni hiyo lilikuwa na mgogoro tangu mwaka 1993 kati ya wamiliki halali na wavamizi ambayo ilikuwa ikisikilizwa kwa nyakati tofauti ambapo mmiliki wake halali alikuwa akishinda lakini watu wanaodaiwa wavamizi wakawa wanaweka pingamizi hadi aliposhinda tena hivi karibuni.

"Baada ya mmiliki halali kushinda kesi hiyo mahakama ilitupa kibali cha kuwaondoa wavamizi ambao tumekuja kwaondoa baada ya kuwapa notisi lakini mfungua kesi hakuweza kuwapa notisi hiyo jambo lililoleta changamoto ya kwa watu waliokuwa wakitumia eneo hilo kushindwa kuokoa vitu vyao" alisema Mbwambo.

Mbwambo alisema mteja wao kwa zaidi ya miaka 20 alishindwa kutumia eneo hilo kwa shughuli zake za uzalishaji mali kutokana na mgogoro.

Mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la James alisema yeye alipangishwa katika eneo hilo kwa kulipa sh.milioni 20 hivyo ameingia hasara kubwa ya ujenzi wa mabanda na vitu vilivyokuwemo ambapo amepoteza zaidi ya sh.milioni 70.

Mfanyabiashara huyo alisema eneo hilo walikuwa wakipangishwa na watu waliouziwa na mtu aliyedai ni lake na miezi michache iliyopita kuna mzee mmoja aliuziwa sehemu ya barabara na kutoa sh.milioni 400 na kujikuta akiingia katika hasara kubwa.

"Tuta watafuta waliotuuzia maeneo katika eneo hilo na kutupangisha ili waweze kuturudishia fedha zetu" alisema James.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.