JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO
MKUTANO WA MHE. NAPE MOSSES NNAUYE, WAZIRI WA HABARI
UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO NA WAANDISHI WA HABARI
TAREHE 20/02/2016
SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA LAPATA BODI MPYA YA
WAKURUGENZI
Dondoo za Kuzungumzia;
Napenda kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake, uundwaji wa Bodi Mpya
umekamilika. Ni vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu wa kisheria wa kuunda
Bodi ya TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa
Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
TBC iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote kwa kazi
waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo. Ninaamini Bodi Mpya
itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita na kubuni mambo
mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.
Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa hii
kuwajulisha yafuatayo;
1. Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E. Mrango kuwa
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza tarehe 19/02/2016 kwa
kipindi cha miaka Mitatu.
Balozi Mrango kielimu ana shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa
Mifumo (MSc – Systems Development) aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini
Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya kwanza ya Takwimu za Kiuchumi katika Chuo
Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.
Balozi Mrango alishashika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu
wa iliyokuwa Wizara ya Miundombinu
Kuanzia Februari, 2011 hadi September, 2013.
Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu. Aidha
nimhakikishie Mwenyekiti huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la TBC liko
chini ya Wizara yangu, tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kuleta
mabadiliko chanya katika shirika letu la Utangazaji.
2.
Kwa mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua
Mwenyekiti wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji, anateua Wajumbe sita wa Bodi. Katika uteuzi
wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilishatupatia
vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.
Hivyo basi, mimi Nape Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni
Sanaa na Michezo, kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili wa
Hazina na kwa kufuata taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua wafuatao
kuwa wajumbe wa Bodi ya TBC;
(i)
Bw. William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi. (M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank
Tanzania ).
(ii)
Bw. Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria. (LLB - UDSM; Associate Director, Litigation & Investment – Bank of Tanzania;
Advocate of the High Court of Tanzania).
(iii)
Bi. Elimbora Abia Muro; Mtaalamu wa Uhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal
Auditor, Tanzania Investment Centre).
(iv)
Bw. Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali watu. (MBA – Public Service
Mgt; Director of Management: President’s
Office – Public Service Management).
(v)
Dkt. Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta
ya Utangazaji na Utangazaji. (PhD – Mass Communication; Associate Dean: School of Journalism, University of Dar Es Salaam)
na
6. Bw. Assah Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta
ya Habari. ( MSc – Media Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information, Culture, Arts and
Sports).
Uteuzi wa wajumbe hawa ni kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka
mitatu.
3. Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi
huu. Tuna matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC
katika tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa
kasi kubwa duniani. Ni imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya
katika utendaji wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika
hili waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania
wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.
Ahsanteni kwa
Kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment