Mhe. Waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumzia uzefu wa Tanzania katika kukabiliana na tatizo la ukeketaji akiwa na wazungumzaji wengine katika Meza Kuu, kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa Burkina Faso Bi. Sika Bella Kabore, Bw. Benoit Kalasi (UNFPA), Bi.Emma Bonino Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Italia.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano na majadiliano kuhusu utokomezaji wa vitendo vya ukeketaji na uhusiano wake na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mkutano huu uliandaliwa kwa pamoja na Wakilishi za Kudumu za Tanzania, Burkina Faso, Italy, Iran, UNFPA na UNCEF
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mhe. Peter Serukamba akifuatilia majadiliano kuhusu tatizo la ukeketaji na adhari zake wa afya na maendeleo ya mtoto wa kike na mwanamke.
Wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi nao wakifuatilia majadiliano yaliyovutia washiriki wengi kuhusu madhara yatokanayo na ukeketaji na namna gani jamii inatakiwa kushirikiana kutokoza tatizo hilo.
Mhe Waziri Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na washiriki wa majadiliano kuhusu ukeketaji.
Waziri Mwalimu akibadilishana mawazo na Waziri mwenzie Sicily Kariuki kutoka Kenya
No comments:
Post a Comment