Habari za Punde

Uchaguzi wa Marudio Wafanyika Zanzibar


Wananchi wa Zanzibar wanashiriki katika Uchaguzi wa marudio ambapo rais wa Zanzibar  baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika 25 Oktoba mwaka jana kufutwa na tume ya uchaguzi.

Uchaguzi huo wa marejeo  unaosimamiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar {ZEC} umetoa nafasi kwa Wananchi wa  Zanzibar kukamilisha kupiga kura kwa nafasi  Tano ikiwemo Rais wa Zanzibar Mwakilishi, Diwani.
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein amepiga kura katika yake katika kituo cha Bungi, Kibele wilaya ya kusini Unguja.
Akizungumza  na wanahabari baada ya kupiga kura amesema anaamini kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na amani.
Mgombea urais wa chama cha ADC Hamad Rashid amepiga kura yake kituo cha Tondooni Wawi wilaya ya Chake-Chake mkoa wa Kusini Pemba na amesema ana  imani ya kuwa Rais au kuwa  Makamu wa Rais wa Zanzibar.
Nae Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi   wamepiga kura katika Kituo chao cha Skuli ya Sekondari ya Kitope Jimbo la Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja mnamo saa 2.4 za asubuhi.

Balozi Seif  anagombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia CCM  katika Jimbo jipya la Mahonda badala ya lililokuwa Jimbo la Kitope.
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura Balozi Seif  amesema ameridhika na zoezi zima liloanza mapema asubuhi na wananchi mbali mbali wameshatumia haki yao ya kupiga kura na kurejea nyumbani kuendelea na shughuli zao za kimaisha.
Balozi Seif  anagombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia CCM  katika Jimbo jipya la Mahonda badala ya lililokuwa Jimbo la Kitope.
Chama cha Wananchi (CUF) hakijashirikia uchaguzi huo kikiamini kuwa kilishinda katika uchaguzi ule wa  Oktoba 25 mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.