Habari za Punde

Zantel Yazindua Mtandao wa Kasi wa 4G Katika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisonge Zanzibar.


Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Balozi Ali Karume, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel bwana Benoit Janin, wakati wa Uzinduzi wa Mtandao wa 4G uliozinduliwa katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisonge Zanzibar.
Wageni Waalikwa wakichati wakati wa Uzinduzi huo wa Mtandao wa 4G Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G uliofanyika katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisonge hapa mjini Zanzibar.

Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mheshimiwa Balozi Ali Karume akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G wa Zantel uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar

Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akionyesha namna mtandao wa 4G unavyofanya kazi kwa kuzungumza kuipitia huduma ya Skype wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G wa Zantel uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar


Msanii Barnaba akitumbuiza wimbo maalumu wa kusherekea uzinduzi wa 4G, wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G wa Zantel uliofanyika katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisonge hapa mjini Zanzibar


Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi iliyounganishwa na mtandao wa 4G Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G wa Zantel uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi iliyounganishwa na mtandao wa 4G Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mheshimiwa Balozi Ali Karume. Anayetazama katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd.


Mfanyakazi wa Zantel akiwaunganisha baadhi ya wateja katika mtandao wa 4G wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.