Habari za Punde

Fainali ya Kombe la Mei Mosi Zeco Mabingwa 2016. kwa Kuifunga Timu ya ZSTC Kwa bao 1--0.

  

  Mhe Haroun Ali Suleiman akizungumza na kutowa Nasaha zake kwa Wachezaji na Wafanyakazi wakati wa mchezo wa Fainali ya Kombe la Mei Mosi lililozikutanisha Timu za ZECO na ZSTC katika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya ZECO imeshinda mchezo huo kwa bao 1--0. na kutawazwa bingwa wa Kombe la Mei Mosi 2016. 
Waziri Mhe Haroun Ali Suleiman akimkabidhi zawadi Refarii Bora wa Michuano ya Mei Mosi kwa mwaka 2016.
Wachezaji wa Timu ya ZSTC wakisalimiana na Mgeni wa heshima wa fainali hiyo ya Kombe la Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa amaan Zanzibar.
Waziri Mhe Haroun Ali Suleiman akimkabidhi Kombe la Ushindi wa Pili wa Michuano ya Kombe la Mei Mosi Kepteni wa Timu ya ZSTC . 
Mabingwa wa Kombe la Mei Mosi Timu ya ZECO wakisalimiana na mgenin rasmin wakati wa mchezo wao wa Fainali ya Kombe la Mei Mosi na kuibuka mabingwa wa Kombe hilo kwa kuifunga Timu ya ZSTC kwa bao 1--0 mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.