Mkuu
wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa Baucha akiongea kwenye hafla hiyo
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo (katikati) akizungumza kwenye hafla ya kupokea msaada wa vifaa kutoka Zantel
Kulia
ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa Baucha na Kushoto ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Dk.Juma Malik.
Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa Baucha (kulia) akimkabidhi vifaa mbalimbali Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo.
Mohamed Mussa Baucha akikabidhi vifaa kwa Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akikabidhi moja ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Zantel kwa Dk.Fadhil Mohamed, Daktari dhamana kanda ya Unguja ambaye pia ni msimamizi mkuu wa kambi za wagonjwa wa kipindupindu
Kampuni ya simu ya mikononi ya Zantel leo
imetoa msaada wa vifaa vya usafi kwa ajili ya kusaidia juhudi za kupambana na
kipindupindu za Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kambi za
kipindupindu visiwani humo.
Vifaa hivyo ambavyo vimekabidhiwa kwa Wizara ya
Afya vimegharimu jumla ya shlingi milioni 11, ni pamoja na matanki ya
kuhifadhia maji, vitanda vya kamba, pampu ya kisima, mabomba ya kunyunyizia
dawa, maturubali mazito, maboksi ya gloves na mafuta ya petroli lita 3,000 kwa
ajili ya magari ya kuhudumia kambi za kipindupindu.
Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo,
Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo amesema ugonjwa wa kipindupindu
ambao mpaka sasa umesabababisha vifo vya watu 53 utatoweka visiwani Zanzibar
baada ya wiki tatu zijazo.
‘Kwa kiasi kikubwa juhudi zetu za kupambana na
kipindupindu kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali zimeanza kufanikiwa, na
tunaomba wadau wengine wazidi kujitokeza kutuunga mkono’ alisema Mahmoud.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya kampuni ya
Zantel, Mkuu wa kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar, Mohammed Mussa amesema
kampuni yake inajivunia kushirikiana na serikali ya Zanzibar kupambana na
ugonjwa wa kipindupindu ambapo ameeleza kuwa tarehe 23 na 24 mwezi uliopita
kampuni ya Zantel imetuma ujumbe kwa wateja wake zaidi ya laki sita na nusu juu
ya kujikinga na ugonjwa huo.
‘Tunawaomba wananchi waendelee kudumisha kanuni
za usafi ikiwemo kuweka mazingira safi, kuchemsha maji ya kunywa, kunawa mikono
kabla ya kula na baada ya kutoka kufanya haja ili kujikinga na janga la
kipindupindu’ alisema Mussa.
No comments:
Post a Comment