Habari za Punde

Bei za Bidhaa Soko la Mwanakwerekwe Zanzibar Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Bei za vyakula vya nafaka katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Mjini Unguja leo kama inavyoonekana pichani bei zake kila bidhaa.    
Bei ya Nazi katika soko la mwanakwerekwe leo bei ya jumla inategemeana na ukubwa wa nazi zimeazia na bei ya shilingi 400/= na 500/= katika soko la jumla skoni hapo na bei ya rejareja inaizwa shilindi 550/= na 700/=

Mjasiriamali katika Soko la Mwanakwerekwe akipanga viazi vitamu fungu moja anauza shilingi 2000/= na 5000/=
Wananchi Kisiwani Unguja wakiwa katika harakati za kujipatia futari katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Unguja, kama walivyokutwa wakiwa katika harakati hizo sokoni hapo leo asubuhi. wakijipatia mahitaji yao kwa ajili ya matumizi ya mwezi mtukufu wa Ramadshani.
Wananchi wakipata futari ya majimbi katika Soko Kuu la Mwanakwerekwe Unguja fungu mmoja la majimbi katika soko hilo linauzwa kati ya shilingi 2000/= na 5000/= .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.