Habari za Punde

Viongozi wa Gewe na Saccos Kisiwani Pemba Wapigwa Msasa.

Mkufunzi kutoka Idara ya vyama vya ushirika Pemba Amini Omar Ali, akiwasilisha mada ya utawala bora, kwa viongozi wa Saccos Pemba, kwenye mafunzo yaliofanyika Michakaini Chakechake Pemba
Afisa Miradi wa GEWE wa kupinga ukatili wa kijinsia kutoka Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA, ofisi ya Zanzibar Asha Abdi Makame, akielezea namna mradi huo unavyoendelea kupinga vitendo hivyo, kwenye mafunzo yaliofanyika Kiuyu Minungwini
Sheha wa shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete Pemba,  Asaa Makame Said  akichangia ripoti ya ukatili wa kijinsia kwenye mkutano wa waratibu na masheha uliofanyika Kiuyu minungwini.
Mjumbe wa ‘Mkombozi saccos’ ya wizara ya maji Pemba, Hamad Muhene Hamad, akiwasilisha kazi za vikundi, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo, yaliofanyika kituo cha waalimu Michakaini Chakechake Pemba
Mjumbe wa ‘Teachers saccos’ ya wizara ya elimu Pemba, Fatma Seif Abeid, akiwasilisha kazi za vikundi, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliofanyika kituo cha waalimu Michakaini Chakechake Pemba
Mjumbe wa ‘Mkombozi saccos’ ya wizara ya maji Pemba, Hamad Muhene Hamad, akiwasilisha kazi za vikundi, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo, yaliofanyika kituo cha waalimu Michakaini Chakechake Pemba
Washiriki wa mafunzo ambao ni wajumbe wa Saccos kisiwani Pemba, wakiwa tuli kusikiliza uwasilishaji wa mada kadhaa. kwenye mafunzo yaliofanyika kituo cha uwalimu Michakaini Chakechake Pemba(Picha na Haji Nassor, Pemba),

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.