Habari za Punde

Wagonjwa 22 bado wanatibiwa kwa Kipindupindu,

 Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr Mohammed Dahoma akizunguma na waandishi wa habari na kuwapa taarifa za maendeleo ya ugonjwa wa Kipindupindu.
Waandishi wa habari wakimzikiliza Mkurugenzi wa Kinga Dr Dahoma alipokuwa akiwapa taarifa kuhusu ugonjwa wa kipindupindu


Jumla ya wagonjwa 22 wameripotiwa kuwepo katika kambi ya kipindupindu kuanzia Mai 28 hadi Juni 3 mwaka huu.

Kuwepo kwa idadi hiyo imeonekana kupungua kwa ugonjwa huo ambapo wiki iliyopita kulikuwa na jumla ya wagonjwa 45.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kinga na ELimu ya Afya Dr Mohammed Dahoma alisema mpaka jana wagonjwa 6 wameripotiwa kisiwani pemba na kwa upande wa Unguja hakuna mgonjwa kwa jana.

Aidha Dahoma alisema wiki iliyopita migahawa saba ilikaguliwa na mitatu kupewa kibali cha kufanya biashara.

Aliitaja migahawa hiyo ni pamoja na Zari Pizza, Rahaleo, na Rama Kiosk yote ipo mkoa wa mjini.

Dr Dahoma aliwashukuru wananchi kwa kuitikia wito wa kudumisha usafi na kuendelea kuwasihi kudumisha usafi kwani ugonjwa huo bado upo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.