Habari za Punde

Wakimataifa Kuanza Kambi Kwa Maandalizi ya Michuano Kombe la FA.

Kikosi cha mabingwa soka Tanzania Bara na mabingwa wa Kombe la FA, Yanga ya jijini Dar es Salaam, kinatarajiwa kuingia kambini Jumatatu, Juni 6. 


Kwa mujibu wa benchi la ufundi, ni kuwa timu inatakiwa kuingia kambini haraka iwezekanavyo ili kuweza kujifua kwa mechi ngumu zilizo mbele yao. 
Benchi hilo lilidai kuwa liliamua kuwapa mapumziko mafupi wachezaji baada ya kufanyakazi kubwa wakitwaa taji la Ligi Kuu na Kombe la FA. 

“Timu itaingia kambini 6 Juni, kujiandaa na michezo yetu ya Shirikisho Afrika, tumekuwa na muda mfupi sana wa kupumzika,”. 

Uongozi umewakubalia kukaa kambini na kwa sasa watu maalum wa ufundi wamepewa kazi ya kujua ni mahali gani kuna hali ya hewa inayofanana na Algeria ili wakaweke kambi huko.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.